UJENZI WA BARABARA VIPANDEVIPANDE WATIA UCHACHU KWENYE HAFLA YA KUKABIDHI MRADI WA BARABARA YA KYERWA KARAGWE KWA MKANDARASI
Powered by Adrian Blog Wananchi wa wilaya ya kyerwa wachukizwa kujengwa kwa lami vipandevipande huku wakiomba Serikali kuunganisha maeneo ya mijini ili kuleta ulinganifu na mwonekano mzuri wa wilaya hayo. Haya yamebainishwa na baadhi viongozi baada ya kusikiliza muhtasari wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kyerwa Karagwe ambayo umetaja kuchukua urefu wa kilometa 50 pekee huku eneo ilo likiwa na zaidi ya kilometa 60. Akiwasilisha taarifa ya mradi Injinia Christian Kayoza, kwa niaba ya mtendaji wa mkuu wa TANROAD amesema kuwa mradi huo utagharimu shilingi bilioni 94.343 bila kodi ya ongezeko la thamani, na mpaka sasa tayari serikali imetoa malipo ya awali kiasi cha shilingi Bilioni 9.3. Mradi huo utachukua Kilomita 50 ambazo ni kutoka Kata ya kyerwa hadi kata ya chonyonyo wilaya ya Karagwe K huku akisema kuwa mradi huu utatekelezwa na fedha za ndani kwa asilimia mia moja. "Mradi huu unatekelezwa kwa kutumia fedha za ndani za jamuhuri ya muungano wa...