Mwalimu wa Maisha na Elimu ya Maisha, Mafanikio



Ulikuwa wakati mzuri na siku mbili zenye ujazo wa mawazo mapya ya aina yake, yenye kubadilisha fikra na mtazamo wa kimaendeleo kama kijana.

Nilikutana na Mr Felix Lufungulo  Felix Lufungulo  Mwalimu mstaafu ambaye ana historia katika kuanzishwa kwa shule moja ya msingi ya Rwamashaju wilayani Kyerwa Pamoja na Kuanzishwa kwa Shule ya Sekondari Nyabishenge.

Makabidhiano ya karatasi ya Product


Kati ya mengi aliyonigusia ni pamoja na kurasa za vitabu vitatu vya Robert Kiyosaki, Mwandishi maarufu wa nchini Marekani, ambavyo ni 
1: Poor_Dady_Rich_dady, The 
2: Cashflow_Quadrant na 
3: The_21st_Century_busness.

Kiyosaki anatumia muda wake mwingi kutazama familia moja ambayo baba wa familia ni mkufunzi wa chuo kikuu lakini kipato chake hakitoshi kukidhi mahitaji yake, familia yake pamoja na kutimiza ndoto zake,

Ila kwa upande mwingine familia ambayo baba wa familia hana elimu kubwa lakini ni fundi gereji lakini ameweza kutimiza ndoto zake nyingi na maisha yake yanamnyokea..

Kiyosaki anajiuliza afanyeje ili aweze kufanikiwa, na anaamua kuuliza maswali pande zote mbili ili alinganishe majibu.

Upande umoja ukasema asome kwa bidii na mwisho wa siku atapata kazi nzuri na maisha yaendelee, huku akimtazama Mkufunzi wa chuo kikuu kama mfano ambaye bado ameshindwa kutimiza ndoto zake kupitia kiasi cha pesa anachokipata kama mshahara wa kila mwezi,

Safari yake ikampelekea kwa familia nyingi ya fundi gereji, akamuuliza swali ilo, akamwambia soma kwa bidii, ukipata kazi fanya serving kidogo na anzisha biashara..

Ukitazama majibu ya watu wote wawili hayakucha elimu, ila kilichoongezeka ni kuwekeza katika biashara, na hapo ndipo unaweza kufikia mafanikio.

Ukitazama maendeleo yapo katika watu wa nyanja nne sana sana ni waajiriwa, wafanyabishara wadogo, wafanyabishara wakubwa pamoja na wawekezaji na kila Sehemu kuna changamoto zake ikiwepo katika wateja pamoja na mitaji,  



Sambamba na hayo pia inakuchukua mda mrefu kutoka katika kuwa mwajiri na kufikia kuitwa mwekezaji, ambapo kwa upambaji wa kawaida inaweza kukuchukua miaka 20 hadi 40..

Maelezo haya yote bwana Robert Kiyosaki aliyaweka katika kitabu chake cha pili ambapo ni " The Cashflow Quadrant" na kueleza namna ambavyo unaweza kutoka stage moja kwenda nyingine.

Lakini katika karne hii ya 21, kumekuwa na mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia hiyo kubadilisha namna tofauti tofauti ya kufanya biashara pamoja na kutoa huduma,

Katika kitabu chake cha tatu ambacho ni " The 21st century Business" amebainisha kuwa katika Sayansi na teknolojia biashara zimehamia katika mitandao hivyo biashara nyingine kuendeshwa kupitia internet ambapo hapa tuna wafanyabishara kama Facebook, twitter n.k pamoja na Networking Marketing ( E commerce) Ambapo hapa tunapata makampuni tofauti tofauti yanayofanya biashara kwa njia ya mtandao na kuigiza kipato kikubwa,,,

Takwimu za biashara za mwaka jana, zimebainisha Networking busness kuongoza katika kuingiza mapato huku Kampuni kama vile movies, michezo, pamoja na zingine zikifuatia,,,

Ni rahisi sana kusema Networking busness pamoja na internet ni ufunguo wa biashara karne ya 21

Powered by Adrian Blog

Comments

Popular posts from this blog