Ijue Bodi Ya Maji Bonde la Ziwa Victoria

Bonde la ziwa Victoria ni eneo ambalo mtiririko wake wa maji unaishia katika ziwa Victoria,  

Wanafunzi wa Mawasiliano ya Uma kutoka SAUT katika picha ya pamoja na PRO wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria
 Engr. Gerald Itimbula
📸SR Janeth

Bonde hili linafuata mipaka ya kihydrojia ( Mtiririko wa maji). Bonde la ziwa Victoria linagusa Mikoa sita ya Tanzania    ambayo ni Kagera, Geiter, Mwanza, Simiyu, Arusha ( Ngorongoro/ ngorongoro creta) Shinyanga ( Kishapu na Shinyanga Vijijini) pamoja na Mkoa wa Tabora ( Wilaya ya Nzega).

 haya yaliundwa na serikali kwa ajili ya kurahisisha usimamizi wa rasilimali maji. na pia kutokana na kuwepo kwa utamaduni tofauti wa njia za utunzaji wa maji katika baadhi ya maeneo hivyo njia rahisi ilikua ni kuyagawa katika mabonde na kuachana na kusimamia kwa mifumo wa kiutawala.

Chombo kinachosimamia Bonde kinaitwa Bodi. Nchini Tanzania kuna Mabonde Tisa (9) na Bodi Tisa za kusimamia, Bodi hizi zipo chini ya idara ya Maji.  Na mojawapo ni Bonde la ziwa Victoria chini ya ( Bodi ya maji Bonde la ziwa Victoria)

Inaongozwa na mkurugenzi wa Bodi ambaye yupo chini ya   mwenyekiti  wa bodi anayeteuliwa na Waziri wa maji  akiwa na wajumbe Tisa. 

Bodi ya Maji ya bonde la ziwa Victoria ipo Chini Ya Mwenyekiti Boniventure Baya.

Bonde la Ziwa Victoria limegawanywa katika catchment ( mabakuli ambayo yanapokea maji kutoka kwenye mto), ambapo  zipo Catchment tatu ambazo ni  Kagera ( Mto Kagera), Mara ( Mto mara)  na  Simuyu ( mto simiyu)  

Kugawanya kwa Bonde katika Catchment zinasaidia katika suala zima la kupata takwimu kwa sababu maji yanayopita katika Catchment ya mto mara ni tofauti na maji yanayopita katika Catchment ya Kagera, hivyo kupitia njia hiyo hudaidia kupata takwimu za maji yanayoingia ziwani kila siku, Pia husaidia kurahisisha usimamizi wa rasilimali maji.

Wanafunzi wa Mawasiliano ya Uma kutoka katika chuo kikuu cha Mt. Augustine ( SAUT)-MWANZA wakiwa mbele ya ofisi ya Bodi ya Maji Bonde La ziwa Victoria May hii leo Mara tu baada ya Semina fupi juu ya namna Bodi inavyofanya kazi
📸Picha na Honest Mwanitega


MAJUKUMU YA BODI

1: Bodi ina majukumu ya kugawa maji kwa njia ya vibali ambapo kuna kibali cha matumizi ya maji, Kibali cha kumwaga Maji taka pamoja na Kibali cha Kuchimba kisima cha Maji. 

Kibali cha matumizi ya maji hutolewa kwa mamlaka za usambazaji maji, Pamoja na Migodi inayohitaji maji kutoka katika vyanzo mbali mbali vya maji kama maziwa na Mito,  mamlaka unahitaji kubainisha ni kiasi gani cha maji  mamlaka husika inahitaj, kwa matumizi gani. Hivyo Mamulaka ina jukumu la kuangalia kama chanzo kinajitosheleza hivyo kutoa kibali hicho. 

Kibali cha matumizi ya maji kinasaidia serikali kufahamu ni kiasi gani cha maji yanatumika kwa siku nchi nzima na nani anatumia pamoja na kuondoa migogoro inayotokana na matumizi ya maji.

 sambamba na hivyo ugawaji wa vibali husaidia kutunza mazingira ambapo maji yakipungua sana yanahijika kubaki maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani pamoja na mazingira,  kupitia tathmini husaidia kujua kiasi cha maji hivyo kujua kama mamlaka maji inayohitaji anasitahili kupewa au hapana.

Sababu za kugawa maji ni kutokana na Sera ya maji ya mwaka 2002 ambapo ilitoa kipaumbele cha ugawaji wa maji katika sehemu tatu ambazo ni Matumizi ya Nyumbani ambayo imepewa kipaumbele kikubwa, pili Mazingira na tatu  social economic activities kama vile viwanda, umwagiliaji n.k

: Hivyo vivyo katika upande wa  kibali cha utupaji taka hutolewa kwa watu wanaoendesha shughuli za viwanda. Kibali cha umwagaji taka kinasaidia kupata mahali pa kutupa taka zinazotoka katika viwanda. Kupitia Kibali hicho takataka hizo hufanyiwa vipimo maalum katika maabara kuona kama zinafika kiwango cha kumwagwa katika chanzo chochote cha  maji.

Pia kibali cha mwisho ni kibali cha kuchimba visima, ambapo kutokana na sheria kwa mtu anaye chimba  Aridhi kwa zaidi ya mita 15 anatakiwa kuomba kibali na kibali hicho kinatolewa na Bodi. Hivyo kuchimba aridhi na kuweka pampu ya kuvuta maji lazima kuomba kibali kwa ajili ya kusimamia na kulinda kiasi cha maji kilichopo chini ya Ardhi

2:P na majukumu hayo Bodi ina wajibu wa kulinda na kutunza mazingira ambapo hupunguza na kumanage uchafuzi katika vyanzo vya maji.

3: Pia kutatua migogoro ya matumizi ya maji. Kazi hii hufanya chini ya Idara ijulikanayo ya ushirikishwaji wa wadau na elimu kwa uma.  ( Stake holder engagement and Public Awareness),Yote kwa yote ili kuamasisha utunzaji wa vyanzo vya maji.

Idara zilizopo ndani ya Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Victoria.

1: Water Bord-   Chini ya Mwenyekiti

2: Basin Director  department ( ya catchment zote)-  ambaye chini yake kina idara tano ambazo ni 

✓Idara ya kufanya tathmini ya wingi wa maji na hali ya maji, 

✓pili  Idara ya Ugawaji maji ( Water Allocation), 

✓tatu Idara ya water resources control and waste management, 

✓ Nne Research trans-boundary and project coordination ( ambayo hufanya tafiti mbalimbali kuhusiana na usimamizi wa maji.

3: Skate holders awareness and public engagement department , ambayo kazi yake ni kutoa elimu kwa uma juu za utunzaji wa vyanzo vya maji.

4:  Human Resources department

5: Account ( monitor all water allocation payments) 

 6: Basin office e department,

Kila Catchment inayotengenezwa inahitaji kuwa na officer  ambapo kwa upande wa binde la ziwa Victoria kuna Catchment ofisi tatu kwa sasa ambazo ni Mwanza, Bukoba na Musoma.

6: Water Users Association ( Jumuia za watumia Maji).

Jumuiya hizi ziliundwa katika ngazi ya vijiji ambavyo vina vyanzo vya maji, kwa mfano katika mto mara imegawanywa katika jumuiya nane. Hiini kwa sababu mnufaika wa kwanza wa maji ni mwananchi.

Kazi zao ni kupanda miti, kuhakikisha hamna mtu anayefanya uchafua maeneo ya vyanzo vya maji, Pamoja na kuchota maji.

Tanzania imegawanyika katika mabonde tisa (9) yakiwa na Bodi Tisa zinazosimamia kila bonde ambazo ni....

Bonde la Pangani,Bonde la  Wami Ruvu ,Bonde la kati, Bonde la Rufiji ( Bonde kubwa),Bonde la Ruvuma na Pwani ya kusini ,Bonde la Nyasa, Bonde la Tanganyika, Bonde la Victoria.

#Sources

https://instagram.com/lake_victoria_basin_tz?igshid=d3sfb9j3ym1x





Comments

Popular posts from this blog