Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Imeupiga Mwingi Miaka 60 Ya Uhuru


Kuelekea maazimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika ambayo baadae ilikuja kuungana na Zanzibar na kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali iliweka utaratibu wa kila wizara kutoa tathmini ya mwelekeo ya wizara yake kuanzia Miaka ya 1961 mpaka sasa,

Jumamosi ya Novemba, 13 wizara wa Utamaduni Sanaa na Michezo iliyopo chini ya waziri Mheshimiwa Innocent Bashungwa, imewakilishwa na naibu waziri wa Wizara hiyo Bi. Paulin Gekulu ambapo amekutana na waandishi wa habari ili kueleza mafanikio, changamoto na mwelekeo wa sekta hiyo katika miaka 60 ya uhuru,

Tangu Tanzania ipate uhuru, Wizara hii imeendelea kuwepo ikiwa na sekta kuu tatu licha ya kuwa sekta hizo zimekuwa zikiwekwa katika wizara mbalimbali, ambapo tumeshuhudia pia kwa mwaka huu Wizara hiyo ilibadilika kutoka kuwa Wizara ya habari utamaduni Sanaa na Michezo na kuwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo,

Katika nchi zote ulimwenguni Utamaduni ndio nguzo mhimu sana katika kutengeneza na kuimaliza misingi ya kimaadili hivyo ata Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliona umuhimu wa kuanzisha Sekta hiyo,

Sambamba na Utamaduni wizara hii inaundwa pia na Sanaa pamoja na michezo ambayo tangu uhuru mpaka sasa vimekuwa nguzo bora katika kuitambulisha Tanzania ulimwenguni,

Katika miaka 60 ya uhuru Mheshimiwa Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Bi Paulin Gekulu ameweka bayana baadhi ya mafanikio pamoja na Changamoto katika sekta hiyo tangu Uhuru mpaka sasa pia kuelezea nini matarajio katika sekta hiyo,

Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma Bi Paulin Gekulu amebainisha kuwa mafanikio katika sekta zote tatu yameifanya Tanzania kuwa katika ramani ya Dunia,

KATIKA UTAMADUNI
Kwa sasa huwezi kutaja Utamaduni wa Tanzania bila Kugusia Kugha ya Kiswahili ambayo iliwaunganisha Watanzania katika kudai uhuru na sasa inaendelea kuunganisha watanzania na kupenya katika maeneo mengi ya Afrika na ulimwengu,

Naibu waziri amesema kuwa wamefanikiwa kukiweka Kiswahili katika Teknolojia ya habari na mawasiliano yaani TEHAMA ambapo ndani ya miaka 60 ya uhuru wamefanikiwa kukifanya kiswahili kutumika katika mifumo ya kompyuta, na kuweka wazi kuwa Kampuni ya Microsoft pamoja na Linux zinatayarisha program za kompyuta ambazo zitakuwa na lugha ya kiswahili, 

Pia Kiswahili kimeweza kutumika katika mashine za kutolea fedha ( ATM) pamoja na Mitandao ya kijamii , huku kikitumika na baadhi mashirika ya ndege katika kutoa huduma za usafiri,

Sambamba na hayo tumeshuhudia kiswahili kikipitishwa kuwa Lugha rasimi katika Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika ( SADC) pamoja na Kiswahili kutumika katika baadhi ya vyuo vya elimu ya Juu katika bala la Ulaya na Amerika hivoyo ni mafanikio Makubwa,

Mafanikio mengine katika utamaduni ni pamoja na kuanzishwa kwa makongamano na vyuo vya Utamaduni kikiwemo chuo cha Utamaduni Bagamoyo ambapo Serikali imesaini mikataba ya kushirikiana na Mataifa mengine ya nje katika kubadilishana ujuzi na Kuimarisha utamaduni wa Kitanzania, Pia kupitia makongamano hayo Wananchi wamepata nafasi ya kuonesha na kuiza kazi zao za mikono za kiutamaduni 

KATIKA SANAA
Ni wazi kuwa sanaa imekuwa nguzo mhimu katika kuimarisha umoja, Ushirikiano na Mshikamano kati ya Tanzania Pamoja na Nchi za nje, Tangu mwaka 1961 Serikali ya Awamu ya kwanza iliona umuhimu wa uwepo wa Shuguli za kisanaa baada ya kuonyeshwa mchango mkubwa katika kuhamasisha kudai uhuru, kupitia sanaa ya nyimbo pamoja na Ngoma, Uchomgaji na uchoraji,

Mafanikio katika Sekta ya Sanaa nchi Tanzania Tangu Uhuru yamechangiwa na kuanzishwa kwa Baraza la Sanaa Tanzania ( BASATA) Mwaka 1984 ikiwa na majukumu ya Kusajili, Kutoa vibali vya shughuli za sanaa, Kutetea Wasanii, Kutafuta masoko ya kazi za sanaa na kuingiza kipato kupitia Sekta ya Sanaa pamoja na kukuza sanaa ambapo kwa mwaka 2018/2019 Sanaa nchini Tanzania ilikuwa kwa asilimia 13.7, Amesema Gekulu

Pia baada ya Kuongezeka kwa changamoto ya wizi wa kazi za baadhi ya wasanii serikali iliamua Kuanzisha Taasisi ya Hakimiliki Tanzania ( COSOTA) mwaka 1999 ikilenga kuwalinda na kuwatetea wabunifu, na kusaidia katika ukusanyaji wa mirabaha itokanayo na Mauzo ya Kazi zao,

Kwa awali kazi ya Sanaa ilionekana kama kazi ya kujiburudisha lakini kazi ya sanaa kwa sasa imekuwa biashara ambapo mpaka kufikia Novemba 2017 watu takribani Milioni 5.5 walikuwa wameajiliwa kupitia Sekta ya Sanaa,

Kutokana na Sekta ya Sanaa na Utamaduni kuwa Muhimu Serikali iliamua kuanzisha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni ( TaSUBa) ambayo kwa sasa imekuwa na mafanikio makubwa na kuwa kituo kilicho tukuka Afrika Mashariki katika Mafunzo ya Utamaduni na Sanaa,

TAKITA UPANDE WA MICHEZO,
Mpaka sasa Michezo miongoni mwa kazi inayofatiliwa zaidi Duniani na Kwa Tanzania ambapo imechukua umakini wa Watanzania wengi mpaka sasa,

Akigusia maendeleo ya Michezo Miaka 60 ya Uhuru Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Bi Paulin Gekulu amesema kuwa Mpaka sasa Tanzania imefanikiwa Kunyakua Medali 16 katika michezo mikubwa Duniani ikiwemo Olympiki, Jumuiya ya Madora na Michezo Barani Afrika na tangu mwaka 1960 Timu za Tanzania zimekuwa zikishiriki bila kukosa,

Kwa kuwa Michezo kwa sasa ni biashara Tanzania pia imefanikiwa kuwa na wachezaji wa kulipwa 54 katika nchi mbalimbali tangu Uhuru, na wachezaji hao wapo katika Mchezo wa Mpira wa Miguu, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu,Kabbadi, Kuogelea pamoja na Mchezo wa Voliboli,

Pia ameongeza kuwa Katika Michezo hiyo ambayo Tanzania imeshika wamefanikiwa Kuchukua Vikombe katika mashindano ya Kimataifa ikiwemo Mpira wa Miguu kwa wanawake ambao wamechukua ubingwa mara 5 katika mashindano ya COSAFA, East Afrika, Pamoja ja CECAFA 

Sambamba na hayo kwa Upande wa Mpira wa Miguu kwa wanaume, Timu zimeshinda na kufuzu kushiriki mashindano kama vile Mashindano ya Kombe la Afrika ( AFCON) kati ya mwaka 1980 na 2019 pia mashindano yA CHAN mara mbili,

Hapo awali kuna baadhi ya michezo ambapo wanawake walikuwa hawapewi nafasi ya kushiriki lakini mpaka sasa wanawake wameweza kujiunga na michezo mingi na kuonesha mafanikio makubwa ambapo mpaka sasa ligi ya wanawake nchini imeanzishwa na pia wanashiriki nkagika ligi za kimataifa,

Watu wenye ulemavu pia wameweza kuhusishwa katika Michezo na wameshiriki katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa na kufanikiwa kupata jumla ya medali 10 za dhahabu, medali 4 za fedha na 3 za Shaba,

Sambamba na mafanikio yaliopatikana je Michezo ya Tanzania ina Taswira gani Kidunia??


Comments

Popular posts from this blog

Amazing Class Tour