UJENZI WA BARABARA VIPANDEVIPANDE WATIA UCHACHU KWENYE HAFLA YA KUKABIDHI MRADI WA BARABARA YA KYERWA KARAGWE KWA MKANDARASI
Powered by Adrian Blog
Wananchi wa wilaya ya kyerwa wachukizwa kujengwa kwa lami vipandevipande huku wakiomba Serikali kuunganisha maeneo ya mijini ili kuleta ulinganifu na mwonekano mzuri wa wilaya hayo.
Haya yamebainishwa na baadhi viongozi baada ya kusikiliza muhtasari wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kyerwa Karagwe ambayo umetaja kuchukua urefu wa kilometa 50 pekee huku eneo ilo likiwa na zaidi ya kilometa 60.
Akiwasilisha taarifa ya mradi Injinia Christian Kayoza, kwa niaba ya mtendaji wa mkuu wa TANROAD amesema kuwa mradi huo utagharimu shilingi bilioni 94.343 bila kodi ya ongezeko la thamani, na mpaka sasa tayari serikali imetoa malipo ya awali kiasi cha shilingi Bilioni 9.3.
Mradi huo utachukua Kilomita 50 ambazo ni kutoka Kata ya kyerwa hadi kata ya chonyonyo wilaya ya Karagwe K huku akisema kuwa mradi huu utatekelezwa na fedha za ndani kwa asilimia mia moja.
"Mradi huu unatekelezwa kwa kutumia fedha za ndani za jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa asilimia 100 na mkandarasi Shamron Lika kutokea China"
Pia ameongeza kuwa mradi huu utachukua kipindi cha miezi 36 ambayo ni takribani miaka mitatu hivyo utakamilika ifikapo mwezi juni 2027.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kyerwa Ndg Daniel Danian wakati akitoa salamu kwa wananchi waliojitokeza katika halfa ya makabidhiano ya mkataba wa ujenzi wa barabara kwa mkandarasi amebainisha kuwa kutoka Kata ya Kyerwa mpaka wilaya ya Karagwe ni takribani kilometa 61,
Hivyo mradi huu utaacha takribani kilometa 11 ili kuunganisha wilaya ya Karagwe hivyo kuomba serikali kutafuta namna ya kukamilisha ili kuleta ulinganifu.
" Hizi kilomita 50, kuna barabara zingine pia inabidi zijengwe. Ingekuwa vizuri mtu akija makao wakuu ya wilaya anakanyaga lami lakini kama kipande huku ni udogo huku ni lami inakuwa haijakaa vizuri".
Pia ameongeza kuwa endapo mradi huu ukikamilika wilaya ya Kyerwa itakuwa na uchumi mkubwa kwani kuna viwanda vingi kwa sasa vinajengwa na barabara itasiadia katika usafirishaji wa malighafi na bidhaa.
" kyerwa hii ni ya uchumi, sisi kama wajumbe wa halmashauri ya Kyerwa na ambavyo tunajenga viwanda vingi kwa ajili ya kuchakata kahawa ili wananchi wa wafanyabishara waweze kuvifikia wanahitaji miundombinu mizuri ya barabara.
Sambamba na hayo Mbunge wa jimbo la kyerwa ambaye ni mwenyeji wa tukio hilo Mhe Innocent Bilakwate ameeleza kuwa, hakuna mradi ambao ametukanwa sana kama mradi wa huo, huku akiitwa muongo, ila leo hii wanakyerwa wanashuhudia mradi ukikabidhiwa kwa mkandarasi.
"Tumeusubiri sana huu mradi ila leo yametimia, tumemsubua sana Rais kuhusu mradi huu wa barabara na hatimaye ametoa fedha kwa ajili ya mradi huu na leo nasema kwangu ni sherehe"
Pia ameongeza kuwa wakati analeta mkandarasi raia wa China kufanya upembuzi yakinifu baadhi ya watu walimtukana kuwa amemleta mchina ili kuwadanganya.
Ikumbukwe kuwa wilaya ya Kyerwa ni moja ya wilaya ambayo ilikuwa haijaunganishwa kwa lami na barabara zingine, huku baadhi ya sehemu zenye mikusanyiko ya watu kama Nkwenda mjini pamoja na Isingro stesheni pamejengwa lami kwa ajili ya kuzuia vumbi maeneo ya biashara, jambo ambalo linawafanya wananchi watamani maeneo yote hayo yaungansihe kwa lami.
Akigusia ilo mkuu wa mkoa wa Kagera Bi Fatuma Abubakary Mwasa amesema kuwa Kyerwa pekee kuna viwanda zaidi ya kumi vunajengwa na kufukia mwakani vitakuwa vimekamilika na kuna wawekezaji wanakuja kujenga hoteli za kisasa na kilichokuwa kinakwamisha ni barabara.
Sambamba na hayo ameeleza kuwa huwa kuna kilometa moja moja ya lami na safari hii wameenda kukaweka hospitali kwa hiyo ili mtu atembee kwenye lami lazima kwanza augue.
"Ukiumwa ndio unaenda kukanyaga lami, mjini pote pakaachwa bila lami, Mheshimiwa tunajua kwenye kapu lako hapaswi kuisha kuna vichenji cheji vinabaki, tunaomba viletwe Kyerwa utupigie lami pale mjini"
Naye Edwin Karegeya ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Rwenkorongo amesema kuwa mradi huo ukikamilika anaiona wilaya ya Kyerwa katika taswira mpya na yenye maendeleo.
" Wilaya yetu imebarikiwa mambo mengi ikiwemo kilimo cha kahawa, hifadhi ila changamoto ya kutokuwa na barabara nzuri inakamisha sana ata wawekezaji wa vyombo vya usafiri na mpaka sasa hatuna mabasi katika wilaya yetu"
Akiongea wakati makabidhiano waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa amesema kuwa Raisi anatambua juu ya kiu ya wanakyerwa kuhitaji sana barabara ya lami, huku akiwashukuru wanakyerwa kwa kuwa na subira mpaka kifikia hatua ya barabara kuanza kujengwa.
Akijibu juu ya takribani kilometa 11 zilizokuwa zikisalia ili kuunganisha barabara ya Omurushaka Karagwe Mhe Bashungwa amesema kuwa tayari ameongeza na Rasi hivyo mkandarasi atamalizia na hizo km 11 ili kuunganishaunganisha moja kwa moja mpaka Murushaka hivyo mradi utakuwa ni jumla Kilometa 61.
"Jana wakati napikea maelekezo ya mh Rais nilimueleza hicho kipande cha kilometa 11 na tayari Mhe Rais ameridhia hivyo Mkandarasi atakapoanza ujenzi kuanzia kata ya Kyerwa asitoke saiti mpaka afike murushaka.
Barabara ya Murushaka kyerwa ndio barabara inayounganisha nchi jirani ya Uganda hivyo wananchi wanakiu kubwa kuona barabara yote inakamilika kwa Kiwango cha lami ili kurahisisha usafiri na usafirishaji. Mhe Bashungwa amesema kuwa Barabara hiyo ya Rwenkorongo Mulongo itaongezwa kwenye ilani mpya ya chama ili kufanyiwa kazi.
Pia ameongeza kuwa hivyo vipande vya hospitali na kuingia mjini atavishughlikia huku anakimwagiza meneja wa TANROAD kufanyia upembuzi yakinifu ili badae zifanyiwe kazi.
Wilaya ya Kyerwa ni moja ya wilaya changa za mkoa wa kagera zilizoanzishwa mwaka 2010 na kulingana na sensa ya mwaka 2022 inakadiriwa kuwa na wakazi zaidi ya laki 4, huku zao lake kubwa la biashara likiwa ni Kahawa
Comments
Post a Comment