Mwalimu wa Maisha na Elimu ya Maisha, Mafanikio
Ulikuwa wakati mzuri na siku mbili zenye ujazo wa mawazo mapya ya aina yake, yenye kubadilisha fikra na mtazamo wa kimaendeleo kama kijana. Nilikutana na Mr Felix Lufungulo Felix Lufungulo Mwalimu mstaafu ambaye ana historia katika kuanzishwa kwa shule moja ya msingi ya Rwamashaju wilayani Kyerwa Pamoja na Kuanzishwa kwa Shule ya Sekondari Nyabishenge. Makabidhiano ya karatasi ya Product Kati ya mengi aliyonigusia ni pamoja na kurasa za vitabu vitatu vya Robert Kiyosaki, Mwandishi maarufu wa nchini Marekani, ambavyo ni 1: Poor_Dady_Rich_dady, The 2: Cashflow_Quadrant na 3: The_21st_Century_busness. Kiyosaki anatumia muda wake mwingi kutazama familia moja ambayo baba wa familia ni mkufunzi wa chuo kikuu lakini kipato chake hakitoshi kukidhi mahitaji yake, familia yake pamoja na kutimiza ndoto zake, Ila kwa upande mwingine familia ambayo baba wa familia hana elimu kubwa lakini ni fundi gereji lakini ameweza kutimiza ndoto zake nyingi na maisha yake yanamnyok...