Posts

Showing posts from November, 2021

Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Imeupiga Mwingi Miaka 60 Ya Uhuru

Image
Kuelekea maazimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika ambayo baadae ilikuja kuungana na Zanzibar na kuunda Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali iliweka utaratibu wa kila wizara kutoa tathmini ya mwelekeo ya wizara yake kuanzia Miaka ya 1961 mpaka sasa, Jumamosi ya Novemba, 13 wizara wa Utamaduni Sanaa na Michezo iliyopo chini ya waziri Mheshimiwa Innocent Bashungwa, imewakilishwa na naibu waziri wa Wizara hiyo Bi. Paulin Gekulu ambapo amekutana na waandishi wa habari ili kueleza mafanikio, changamoto na mwelekeo wa sekta hiyo katika miaka 60 ya uhuru, Tangu Tanzania ipate uhuru, Wizara hii imeendelea kuwepo ikiwa na sekta kuu tatu licha ya kuwa sekta hizo zimekuwa zikiwekwa katika wizara mbalimbali, ambapo tumeshuhudia pia kwa mwaka huu Wizara hiyo ilibadilika kutoka kuwa Wizara ya habari utamaduni Sanaa na Michezo na kuwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Katika nchi zote ulimwenguni Utamaduni ndio nguzo mhimu sana katika kutengeneza na kuimaliza misingi ya kimaadili hivy...